KATIBU Tawala mpya wa Mkoa wa
Simiyu, Miriam Mmbaga, ameahidi kutoa ushirikiano kwa watumishi mkoani humo isipokuwa
kwa watakaojihusisha na vitendo vya wizi na utovu wa nidhamu ambao amesema
hatasita kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria.
Mmbaga ameyasema hayo jana Julai 8,
2020 wakati wa makabidhiano ya ofisi kutoka kwa aliyekuwa Katibu Tawala wa
Mkoa huo, Jumanne Sagini.
Aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini (mwenye suti ya buu kulia) akimkabidhi baadhi ya nyaraka za ofisi kwa Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa huo, Miriam Mmbaga |
Kwa upande wake, Sagini amewapongeza
watumishi wa ngazi mbalimbali mkoani hamo kutokana na ushirikiano ambao
wamekuwa wakimpa tangu alipoteuliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli mwaka
2016, hatua iliyosababisha kusukuma mbele maendeleo ya mkoa huo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, amemshukuru Sagini kwa namna alivyosimamia maelekezo ya serikali na kuhakikisha kuwa mkoa huo unapiga hatua kimaendeleo.
"Watanzania tujenge utamaduni wa
kuwasifia watu wakiwa hai na sio mtu akifa ndio asifiwe, kwa kweli tunajivunia
uwepo wa katibu tawala aliyemaliza muda wake," amesema Mtaka.
(Imeandikwa na Anita
Balingilaki, Simiyu)
"
No comments:
Post a Comment