NEWS

Thursday 9 July 2020

RAS mpya Simiyu atoa msimamo wa kiutendaji


KATIBU Tawala mpya wa Mkoa wa Simiyu, Miriam Mmbaga, ameahidi kutoa ushirikiano kwa watumishi mkoani humo isipokuwa kwa watakaojihusisha na vitendo vya wizi na utovu wa nidhamu ambao amesema hatasita kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria.

Mmbaga ameyasema hayo jana Julai 8, 2020 wakati wa makabidhiano ya ofisi kutoka kwa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa huo, Jumanne Sagini.
Aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini (mwenye suti ya buu kulia) akimkabidhi baadhi ya nyaraka za ofisi kwa Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa huo, Miriam Mmbaga 
Kwa upande wake, Sagini amewapongeza watumishi wa ngazi mbalimbali mkoani hamo kutokana na ushirikiano ambao wamekuwa wakimpa tangu alipoteuliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli mwaka 2016, hatua iliyosababisha kusukuma mbele maendeleo ya mkoa huo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, amemshukuru Sagini kwa namna alivyosimamia maelekezo ya serikali na kuhakikisha kuwa mkoa huo unapiga hatua kimaendeleo.

"Watanzania tujenge utamaduni wa kuwasifia watu wakiwa hai na sio mtu akifa ndio asifiwe, kwa kweli tunajivunia uwepo wa katibu tawala aliyemaliza muda wake," amesema Mtaka.

 (Imeandikwa na Anita Balingilaki, Simiyu)
"

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages