NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mwita Waitara amefanya ziara katika Jimbo la Tarime Vijijini na kuhimiza watendaji wa serikali kusimamia ili kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo ya wananchi inayotekelezwa jimboni humo na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Ilani ya CCM inakamilika kwa wakati.
Katika
ziara hiyo ya jana Julai 8, 2020, Waitara amekagua maendeleo ya ujenzi na
ukarabati wa miundombinu mbalimbali ya shule za msingi na sekondari katika kata
za Binagi, Nyarero, Pemba, Mbogi, Ganyange, Nyakonga na Nyamwaga.
Naibu
Waziri wa Tamisemi, Mwita Waitara (katikati mwenye suti), akikagua maendeleo ya
ujenzi wa choo katika Shule ya Msingi Soroneta
Akizungumza
na makundi ya wananchi wa maeneo hayo wakiwamo walimu, madiwani, wanafunzi,
watendaji wa kata na viongozi wa CCM kwa nyakati katika tofauti baada ya
kukagua miradi hiyo, Naibu Waziri huyo amesema mbali ya Serikali ya Awamu ya
Tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kuidhinisha elimu ya msingi na
sekondari bila malipo, imetoa fedha za kugharimia uboreshaji wa mazingira ya
wanafunzi kujifunza na kujifunzia.
Waitara
wamewataka walimu wakuu kushirikiana na wataalamu wa idara husika na watendaji
wa vijiji na kata kusimamia ili pia kuhakikisha kuwa miradi hiyo inatekelezwa
kwa kiwango cha ubora uliokusudiwa.
No comments:
Post a Comment