KADA kijana wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Jafari W. Chege, ametangaza nia ya kugombea ubunge Rorya kwa
dhamira ya kujenga mfumo wa kuinua kipato cha kila mkazi wa jimbo hilo kupitia
sekta mbalimbali.
Chege ambaye ni mzaliwa wa
kijiji cha Nyihara katika kata ya Kyang’ombe wilayani Rorya, amesema
akifanikiwa kuteuliwa na CCM na baadaye kupata ridhaa ya wananchi ya kuwa
mbunge wa Rorya, ataelekeza nguvu kubwa katika kuhakikisha Wanarorya
wananufaika ipasavyo na shughuli za kilimo, uvuvi na mifugo, lakini pia kuwaondolea
adha katika huduma za maji, afya na elimu.
No comments:
Post a Comment