NEWS

Saturday 22 August 2020

Tiboche sasa rasmi kugombea udiwani Nyanungu

Tiboche Richard Rokomo (kushoto) akipokea fomu ya kugombea udiwani wa kata ya Nyanungu kutoka kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi katani humo leo

KADA kijana wa CCM na msomi wa chuo kikuu, Tiboche Richard Rokomo, leo Jumamosi Agosti 22, 2020 amechukua fumo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kugombea udiwani katika kata ya Nyanungu, jimbo la Tarime Vijijini.

 

Tiboche ameteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika kinyang’anyiro hicho ambapo chama hicho kinaamini ana uwezo wa kuikomboa kata hiyo ambayo umeongozwa na upinzani kwa miaka 15.

 

Katika uchukuaji wa fomu kwenye ofisi ya Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Nyanungu, Tiboche ameambatana na mke wake, Angel Mataro na kusindikizwa na  wanachama na wapenzi wa chama hicho tawala.

Tiboche Richard Rokomo akipungia wananchi mkono wakati alipokwenda kuchukua fomu ya kugombea udiwani wa kata ya Nyanungu. Kulia ni mke wake, Angel Mataro
 

Tiboche ambaye pia Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Tarime, ni mhitimu wa Shahada ya Sayansi ya Hesabau na Kompyuta katika Chuo Kikuu cha Iringa.

 

Katika kinyang’anyiro hicho, Tiboche atachuana na Gichonge Sigara anayetajwa kuteuliwa na Chadem kugombea udiwani wa kata hiyo.

 

(Imeandikwa na Mara Online News, Tarime)

1 comment:

  1. Nakutakia kila lakheri ndugu, mungu akutangulie kwa kila hatua,, 2getherwecan.

    ReplyDelete

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages