NEWS

Saturday 14 November 2020

Serengeti Safari Marathon yafana hifadhini

Baadhi ya wakimbiaji wakishiriki mbio za Serengeti Safari Marathon ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti leo asubuhi.

 

MASHINDANO ya mbio za Serengeti Safari Marathon yamefanyika kwa mvuto wa aina yake ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) eneo la Ndabaka Gate leo Novemba 14, 2020 kwa mbio za kilomita 5, 10, 21 na 42.

Sehemu nyingine ya wakimbiaji wakishiriki mbio za Serengeti Safari Marathon ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti leo asubuhi.

 

Mashindando hayo yameshirikisha watalii kutoka mataifa mbalimbali, wanariadha kutoka mikoa ya Mara, Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Dar es Salaam, Arusha na Kilimanjaro, viongozi na watumishi wa Serikali, SENAPA na Shirika la Frankfurt Zoological Society (FZS).

Viongozi wa mkoa wa Mara, TANAPA, SENAPA na wapenzi wa uhifadhi wa wanyamapori wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti leo.

 

Baadhi ya viongozi walioshiriki mashindano hayo ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Regine Hess na Kamishna wa Uhifadhi TANAPA ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt Allan Kijazi,

 

Viongozi wengine ni Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Caroline Mthapula, Msimamizi wa miradi ya wafadhili FZS, Michael Thompson, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Kanda ya Magharibi, Martin Loiboki na Mhifadhi Mkuu wa SENAPA, Masana Mwishawa, Meneja Mradi FZS Serengeti, Masegeri Rurai.

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Regine Hess (wa tatu kulia), Msimamizi wa miradi ya wafadhili FZS, Michael Thompson (wa pili kulia), Meneja Mradi FZS Serengeti, Masegeri Rurai (wa nne kulia) na wafanyakazi wa shirika hilo ni miongoni mwa washiriki wa mbio za Serengeti Safari Marathon ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti leo asubuhi.

 

Mwishawa amesema mashindano hayo ya Serengeti Safari Marathon yamewashirikisha wakimbiaji zaidi ya 1,000, wengi wao wakiwa vijana wa jinsia zote.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (wa pili kushoto), akiongozwa na wakuu wa mikoa, Adam Malima wa Mara na Anthony Mtaka wa Simiyu, kuingia eneo la Ndabaka Gate ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti zilikofanyika mbio za Serengeti Safari Marathon leo.


 

Mgeni rasmi wa mashindano hayo ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Tanzania, Jakaya Kikwete.

 

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages