NEWS

Thursday, 8 January 2026

Waziri Nyansaho atembelea Kamandi za Jeshi la Wananchi wa Tanzania



Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi wa Kamandi za Jeshi jijini Dar es Salaam jana.

Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
-------------------

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, jana aliendelea na ziara yake ya kikazi kwa kutembelea kamandi mbili za vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi na Kamandi ya Wanamaji jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo, Waziri Nyansaho alipokewa na Mkuu wa Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi, Meja Jenerali Iddi Nkambi ambaye alimpa taarifa ya utekelezaji wa majukumu wa kamandi hiyo.

Aidha, akiwa katika Kamandi ya Wanamaji, Waziri Nyansaho alitembelea meli za kivita na karakana ya meli vita ambapo alizungumza na maafisa wanadhimu wa Kamandi hizo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages