NEWS

Tuesday 16 February 2021

DC Msafiri asimamia ufyekaji, uteketezaji bangi Tarime

Mkuu wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Mhandisi Mtemi Msafiri (katikati ya askari polisi) akisimamia ufyekaji bangi kijijini Kwisarara.

MKUU wa Wilaya (DC) ya Tarime mkoani Mara, Mhandisi Mtemi Msafiri ameendelea kuwataka wananchi kuachana na kilimo na biashara ya zao haramu la bangi ili kuepuka mkono wa sheria.

 

Badala yake, amewahimiza wananchi wilayani humo kuelekeza nguvu katika kilimo cha mazao halali ya chakula na biashara.

DC Msafiri akiendelea kusimamia ufyekaji wa bangi kijijini Kwisarara.

Mhandisi Msafiri ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Tarime, amesisitiza hayo leo Februari 16, 2021 katika kijiji cha Kwisarara alikokwenda kusimamia ufyekaji na uteketezaji wa bangi mbichi shambani.

Bangi hiyo ikiteketezwa kwa moto.

DC huyo amefuatana na askari polisi katika tukio hilo la kushtukiza. Mtuhumiwa wa shamba hilo anatafutwa.

 

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages