NEWS

Thursday 15 July 2021

LHRC yakutanisha wadau tena kujadili migogoro Tarime

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kupitia Mradi wa Jenga Amani Yetu, leo Julai 15, 2021 kimewakutanisha wadau, wakiwemo watumishi wa serikali, asasi za kiraia na waandishi wa habari, kufanya tathmini, kujadili na kukumbushana vyanzo vya migogoro mbalimbali katika jamii wilayani Tarime, Mara.

Aidha, wadau hao wamejadili kuhusu suluhusho la migogoro hiyo, huku maofisa wa LHRC wakitumia nafasi hiyo pia kuwakumbusha kutumia fursa zilizopo kupata ruzuku zinazotolewa na mradi huo.
 
Mradi huo wa Jenga Amani Yetu unatekelezwa na LHRC kwa ushirikiana na ZLSC na SFCG, kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).

MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages