NEWS

Sunday 25 February 2024

Ajali yagharimu maisha ya watu 25 mkoani Arusha, Rais Samia atuma salamu za pole kwa familia, ndugu




Na Mwandishi Wetu
----------------------------


WATU 25 wakiwemo raia wa kigeni watatu, wameripotiwa kufa katika ajali ya magari manne iliyotokea jana jioni katika eneo la Ngaramtoni mkoani Arusha.

Ajali hiyo inadaiwa kusababishwa na lori lililokatika breki na kisha kugonga magari mengine madogo.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni wanaume 14, wanawake 10 na mtoto, na waliojeruhiwa ni 21 wakiwemo wanaume 14 na wanawake saba.

Kufuatia tukio hilo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole akielezea kupokea kwa masikitiko taarifa hiyo.

“Natuma salamu za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa waliopoteza jamaa zao katika ajali hii. Ajali hizi zinachukua wapendwa wetu, nguvu kazi ya Taifa na mihimili ya familia. Naendelea kutoa wito kwa kila mmoja kuzingatia sheria za usalama barabarani katika matumizi ya vyombo vya moto.

“Naagiza vyombo vyetu vya ulinzi, usalama na udhibiti kuendelea kuhakikisha vinasimamia sheria kikamilifu, ikiwemo ukaguzi wa mara kwa mara wa vyombo vya usafiri na udhibiti wa leseni kwa madereva wanaorudia kuvunja sheria mara nyingi na wakati mwingine kusababisha watu kupoteza maisha.

“Mwenyezi Mungu azilaze roho za ndugu zetu hawa mahali pema peponi. Amina,” amesema Rais Samia.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages