NEWS

Sunday, 28 July 2024

Ajali ya gari yaua mtalii wa kigeni Hifadhi ya Serengeti




Na Mwandishi Wetu
----------------------------

Mtalii wa kigeni mwenye asili ya China amefariki dunia na wenzake sita kujeruhiwa baada ya gari (pichani juu) walilokuwa wakitumia kupata ajali ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti.

Taarifa kwa umma iliyotokewa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) imesema ajali hiyo iliyokea jana Julai 28, 2024 saa 10 jioni, wakati gari hilo lenye namba za usajili T 603 DCL mali ya Kampuni ya Yonda Afrika likiwa njiani kurudi Hoteli ya Lobo Wildlife.

“Gari hilo lilikuwa na watalii saba wenye asili ya China na dereva raia wa Tanzania. Mmoja wa wageni hao alifariki dunia na wengine sita walipata majeraha.

“Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mugumu [wilayani Serengeti] na majeruhi sita wanaendelea kupata matibabu katika hospitali hiyo.

“Uchunguzi unaendelea kwa kushirikiana na mamlaka zingine ili kubaini chanzo cha ajai hiyo,” imesema taarifa hiyo iliyosainiwa na Afisa Uhifadhi Mkuu Kitengo cha Mawasiliano – TANAPA, Catherine Mbena.
Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages