NEWS

Monday, 15 July 2024

Mwenyekiti UVCCM Mara: Sauti ya Mara mnafanya vizuri kutangaza habari chanya za wawekezaji waliopo ndani ya mkoa



Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mara, Mary Daniel Joseph (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mhariri Mtendaji wa Mara Online News na Gazeti la Sauti ya Mara, Mugini Jacob, wakati Mary alipotembelea ofisi za vyombo hivyo vya habari mjini Tarime, mapema leo Julai 15, 2024. (Picha na Mara Online News)
--------------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Tarime
-------------------------------------

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mara, Mary Daniel Joseph amesema umoja huo unafarijika kuona Gazeti la Sauti ya Mara na chombo chake dada cha Mara Online News, vinazipa kipaumbele habari zinazowatia moyo wawekezaji katika mkoa huo.

“Nipongeze kazi nzuri inayofanywa na Sauti ya Mara, Mara Online News na Lake Zone Watch kwa kuonesha maendeleo na mambo mazuri yanayofanywa na wawekezaji katika mkoa wetu wa Mara.

“Mfano tunaona habari za miradi ya CSR (Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii) na minginge mbalimbali ya maendeleo inayofanywa na wawekezaji. Hii inawatia moyo wawekezaji kuliko kuandikwa kwa mabaya tu hata kama wanafanya mazuri,” amesema Mary alipotembelea ofisi za vyombo hivyo vya habari mjini Tarime, mapema leo Julai 15, 2024.

Mhariri Mtendaji wa Sauti ya Mara, Mugini Jacob (kushoto) na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mara, Mary Daniel Joseph wakiendelea na mazungumzo ofisini. (Picha na Mara Online Newes)
------------------------------------------------

Mary ameongeza kuwa vyombo hivyo vya habari vinajitahidi kusaidia kubadilisha taswira na mitizamo hasi juu ya wawekezaji na wadau wengine wa maendeleo iliyokuwepo siku za nyuma.

“Vyombo hivi vinafanya kazi nzuri na kubwa sana ya kutangaza taswiara halisi ya mkoa wa Mara, wadau wa maendeleo wakiwemo investors (wawekezaji) ambao wamekuwa wakiandikwa negatively (vibaya). Mmetufanya UVCCM tujue umuhimu wa media [vyombo vya habari], mmekuwa mfano mzuri,” amesema Mary.

Kiongozi huyo wa UVCCM Mkoa amesema pamoja na changamoto zilizopo Mara, lakini pia kuna mambo mazuri na fursa nyingi za uwekezaji zinazostahili kutangazwa ili kusaidia kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika mkoa huo. “Mara sio mkoa wa hovyo kama inavyozungumzwa,” amesisitiza.

Kwa upande wake Mkurugenzi na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Sauti ya Mara, Mugini Jacob amemshukuru Mary kwa kutembea ofisi za vyombo hivyo na kumuahidi ushirikiano chanya utakaosaidia kuhamasisha maendeleo ya wana-Mara wakiwemo vijana.

“Tunakushukuru Mary kwa kututembelea, tumepokea pongezi zako, umetia moyo wa kuendelea kufanya vizuri zaidi kwenye tasinia ya habari na kuwa sehemu ya wadau ambao watauweka mkoa wa Mara katika ramani ya dunia kimaendeleo,” Jacob ambaye pia Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara amemueleza Mwenyekiti huyo wa UVCCM Mkoa wa Mara.

Mara ni mkoa ambao unatajwa kuwa na fursa nyingi za kipekee ambazo zikikitumika vizuri zinaweza kufanya mageuzi makubwa ya maendeleo ya kisekta katika mkoa huo ambako ndiko alikozawaliwa na kuzikwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Miongoni mwa fursa hizo ni kilimo cha kahawa aina ya Arabica ambayo inaripotiwa kutamba kwa ubora katika soko la dunia.

UNAWEZA PIA KUSOMA:

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages