NEWS

Tuesday, 16 July 2024

Mamlaka zanasa watuhumiwa wawili, magunia 205 ya dawa za kulevya Mara




Na Mwandishi Wetu, Bunda
-------------------------------------

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, limekamata magunia 205 (pichani juu) yakiwa na majani makavu yanayodhaniwa kuwa zao haramu la bangi.

Aidha, jeshi hilo linawashikilia watu wawili waliokutwa wakisafirisha magunia hayo kwenye gari la mafuta kutoka mkoani Mara kwenda jijini Dar es Salaam.

Ukamataji huo ulifanyika wilayani Bunda jana, ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt Vicent Naano alikemea uhalifu huo akisema mamlaka zimejipanga kuwadhibiti wakulima, wasafirishaji na wafanyabiashara ya dawa za kulevya mkoani Mara.

Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages