Baadhi ya mabasi ya abiria yaliyozuiwa Nyamikoma wilayani Busega leo.
------------------------------------------------
Na Mwandishi Wetu
---------------------------
---------------------------
Mamia ya abiria wanaripotiwa kuzuiwa na wananchi kuendelea na safari katika eneo la Nyamikoma wilayani Busega, Simiyu baada mwanafunzi kudaiwa kugongwa na gari katika eneo hilo mapema leo Julai 15, 2024.
Taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka eneo la tukio zinadai kuwa wananchi hao ambao wamefunga barabara hiyo kwa saa kadhaa, pia wametumia mawe kushambulia baadhi ya mabasi ya abiria yaliyokuwa yakitoka mkoani Mara kuelekea jijini Mwanza.
“Yaani tangu saa tatu tumekwama hapa, wananchi wanarusha mawe, polisi wamepiga mabomu lakini wamezidiwa,” mmoja wa abiria wa basi linalofanya safari kati ya Tarime mkoani Mara na jijini Mwanza ameiambia Mara Online News kwa njia ya simu.
Baadhi ya abiria wakiwa katika taharuki baadaya mabasi waliyokuwa akitumia kuzuiwa Nyamikoma.
--------------------------------------------
Mara Online News inaendelea kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kuzingumzia tukio hilo.
No comments:
Post a Comment