NEWS

Sunday 11 August 2024

Furahia 88 Family & Derby Day ilivyovutia watalii wa ndani Hifadhi ya Kisiwa cha Saanane



Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda (kushoto) akisalimiana na mmoja wa watalii waliotembelea Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane. Mwenye fulana ya bluu nyuma yake ni Mkuu wa Hifadhi hiyo, Tutindaga George.
--------------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Mwanza
----------------------------------------

Furahia 88 Family & Derby Day imeweka historia ya pekee kwa kuwavutia watalii wa ndani, wakiwemo mashabiki wa timu za Simba SC na Yanga SC katika Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane iliyopo Ziwa Victoria jijini Mwanza.

Ilikuwa siku maalum na ya kipekee zaidi ndani ya hifadhi hiyo, ambapo mashabiki hao walifurahia usafiri wa boti ndani ya Ziwa Victoria na kushuhudia ‘live’ mtanange wa timu hizo.
Watalii wakiwemo mashabiki wa Simba na Yanga wakifurahia mandhari ya kuvutia ndani ya Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane.
------------------------------------------------


Awali, watani hao wa jadi walianza kufanya ziara ya kitalii na kujionea vivutio vya wanyamapori wa aina mbalimbali ndani ya Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane.

Ziara hiyo ilifunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda ambapo watalii 139 walijitokeza kufanya utalii na kutazama mtanange huo wa Simba na Yanga.
RC Mtanda akisalimia na wahifadhi.
-----------------------------------------------

Mtanda alituma wito kwa wakazi wa Mwanza kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya mkoa huo, ikiwemo Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane.

Aidha, alilishauri Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kubuni vivutio vipya vya utalii ili kushawishi watalii wengi zaidi kupanga kutembelea hifadhi hiyo na jiji la Mwanza kwa ujumla.
Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages