Kufukuza kuku ni miongoni mwa mashindano yaliyohusisha wanafunzi kutoka shule za sekondari 10 katika bonanza lililoandaliwa na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Ingwe wilayani Tarime jana Agosti 8, 2024.
----------------------------------------------
--------------------------------------
Wanafunzi wa shule za sekondari 10 wameshiriki mashindano ya michezo mbalimbali ikiwemo kuimba na kufukuza kuku katika bonanza lililoandaliwa na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, kaskazini mwa Tanzania.
Bonanza hilo lilifanyika jana Agosti 8, 2024 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Ingwe, lengo kuu likiwa kutoa elimu juu ya faida za mgodi huo kwa jamii zinazouzunguka na taifa kwa ujumla.
Lengo lingingine lilikuwa kuelimisha jamii kuhusu madhara ya vitendo vya kuvamia mgodi huo, lakini pia umuhimu wa kutunza mazingira na kudumisha uhusiano kati ya jamii na mgodi huo.
Shule za sekondari zilizoshiriki katika bonanza ni Nyamongo, Matongo, Genge, Kemambo, JK Nyerere, Bwirege, Ingwe, Kibasuka, Nyabichune na Nyamwaga Hill.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, Apolinay Lyambiko akimvalisha mwanafunzi miwani maalumu. Wa pili kutoka kulia ni Meneja Mahusiano wa Mgodi huo, Francis Uhadi.
Safarani Msuya kutoka Idara ya Mahusiano ya Mgodi wa Dhahabu wa North Mara akigawa taulo za kike kwa wanafunzi.
---------------------------------------------
Hatua hizo za mgodi wa North Mara ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kuendeleza sekta ya elimu.
"Tumewekeza sana kwenye elimu, mazingira pamoja usalama. Mgodi umekuwa ukichangia bilioni 4.5 [shilingi] kila mwaka. Mpaka sasa bilioni 22 zimeenda kwenye miradi 250, hususan kwenye miundombinu ya elimu.
"Tuna mpango wa kupanua mradi wa maji kwenda kwenye vijiji vilivyobakia, tunalipa kodi na mirahaba tangu uzalishaji ulivyoanza.
“Kupitia North Mara Trust Fund, wanafunzi wamekuwa wakilipiwa gharama za masomo ambapo mpaka sasa tumeshalipia wanafunzi 500 wanaosoma katika vyuo mbalimbali. Lakini pia tunalipa service leavy (ushuru wa huduma).
“Tunataka watu wajifunze umuhimu wa uwepo wa mgodi huu, tunahamasisha wanafunzi kuweka mkazo kwenye elimu, nasi pia [mgodi] tuendelea kuweka mkazo kwenye elimu,” alisema Meneja Mkuu wa mgodi huo, Apolinary Lyambiko.
“Bonanza hili limekuwa elimu kwetu, tumeelimishwa umuhimu wa uwekezaji wa mgodi huu na faida zake kwa jamii, lakini pia tumeelimishwa umuhimu wa kutunza mazingira.
“Vile vile tumefahamishwa fursa mbalimbali za kuwezesha wananchi kunufaika zaidi na mgodi huu, hivyo tunakwenda kuwa mabalozi wazuri katika jamii zetu,” alisema mwanafunzi Nyamisi Bwele kutoka Shule ya Sekondari Ingwe.
Mwanafunzi Nyamisi Bwele kutoka
Shule ya Sekondari Ingwe.
--------------------------------------
Mgodi wa Dhahabu wa North Mara unaendeshwa na Kampuni ya Barrick Gold kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.
No comments:
Post a Comment