NEWS

Sunday 8 September 2024

Rais Samia ateua Wakurugenzi Wakuu wapya TCAA, TAA



Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, 
Dkt Samia Suluhu Hassan.
--------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amemteua Salim Ramadhani Msangi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), nafasi ambayo alikuwa akiikaimu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt Moses Kusiluka, Rais Samia pia amemteua Abdul Athumani Mombokaleo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).

“Kabla ya uteuzi huu, Mombokaleo alikuwa Meneja wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), anachukua nafasi ya Mussa Mbura ambaye atapangiwa majukumu mwengine,” imehitimisha taarifa hiyo iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Sharifa Nyanga.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages