
Wadhamini wa Kongamano la Tano la Idhaa za Kiswahili Duniani, akiwemo mwakilishi wa Nyambari Nyangwine Group katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Arusha
----------------
Kampuni ya Nyambari Nyangwine Group imetunukiwa cheti maalum cha shukurani kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake wa udhamini uliosaidia kufanikisha Kongamano la Tano la Idhaa za Kiswahili Duniani.
Nyambari Nyangwine Group imekabidhiwa tuzo hiyo katika Kongamano hilo ambalo limefanyika kuanzia Machi 24 hadi 27, 2026 kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).

Mwakilishi wa Nyambari Nyangwine Group akionesha cheti cha shukurani walichotunukiwa na BAKITA
Kwa mujibu wa BAKITA, mchango wa Nyambari Nyangwine Group ulikuwa wenye tija katika kufanikisha maandalizi na uendeshaji wa kongamano hilo.
Nyambari Nyangwine Group imeona fahari kuchangia udhamini wa kongamano hilo ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuhamasisha na kuendeleza Kiswahili ili kuhakikisha kinakuwa moja ya lugha kuu zinazotumika duniani katika mawasiliano, elimu na biashara.

Washiriki wa kongamano hilo wamejadili nafasi na umuhimu wa lugha ya Kiswahili katika vyombo vya habari, teknolojia ya mawasiliano na maendeleo ya kijamii na kiuchumi duniani.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa kongamano hilo alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, ambaye aliongozwa na mwenyeji wake, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda.

Sehemu ya banda la Nyambari Nyangwine Group la maonesho ya vitabu katika kongamano hilo

No comments:
Post a Comment