NEWS

Saturday, 11 January 2025

Dk Angela Tabiri: Malkia wa hesabu wa Ghana anayeng'aa Kimataifa

Pichani ni Dk Angela Tabiri,Mwafrika wa kwanza kushinda shindano la Big Internet Math Off
-----------------------------------
Akijulikana nchini Ghana kama Malkia wa Hesabu, Dk Angela Tabiri ndiye Mwafrika wa kwanza kushinda shindano la Big Internet Math Off, mafanikio makubwa kabisa kwa mtu ambaye hakuwa amepanga kusoma hisabati.

Mghana huyo mwenye umri wa miaka 35 "anafurahia kutatua mafumbo na maswali ya hesabu" na ana matumaini kuwa ushindi wake wa mwaka 2024 utafungua ulimwengu wa hisabati kwa wanawake wengine wa Kiafrika ambao kwa kawaida wamekata tamaa ya kujikita kwenye mada hiyo.

Wanahisabati kumi na sita walialikwa kushindana kumpata "mtaalamu wa hisabati wa kuvutia zaidi duniani", tukio la upigaji kura ya umma lililoanzishwa katika 2018 na blogu ya Aperiodical.

Mshindi wa kwanza alikuwa Dr Nira Chamberlain, mtaalamu wa kwanza mweusi wa hisabati kujumuishwa katika kitabu cha kumbukumbu cha Uingereza 'Who's Who' na makamu wa rais wa bodi ya wataalamu ya Institute of Mathematics and its Applications.
Chanzo:BBC
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages