NEWS

Monday, 13 January 2025

Marekani: Moto waua wakazi 24 Los Angeles




Los Angeles - Moto wa nyika unaowaka na kuteketeza kila kitu kilicho mbele yake, kama ilivyoandikwa katika Biblia Takatifu kuhusu kuteketezwa kwa mji wa Sodoma na Gomora, hadi kufikia leo ulikuwa umeua watu 24 katika jiji la Los Angeles, Jimbo la California, Marekani.

Baadhi ya watu wameubatiza moto huo kuwa wa ‘Muujiza’ kwa sababu pamoja na jitihada kubwa za kuuzima, ndivyo unavyozidi kulipuka na kuunguza kila kitu na kuwaacha watu midomo wazi!

Kwa mujibu wa Idara ya Tiba na Uchunguzi ya Kaunti ya Los Angeles, licha ya vifo 24 vilivyoripotiwa, inasemekana watu kadhaa katika jiji hilo kubwa la Marekani hawajulikani walipo.

Hadi kufikia jana wazima moto waliendelea na jitihada za siku sita za kupambana na moto huo huku ukizidi kuzizima kutokana na upepo mkali unaovuma kwa kasi isiyomilithilika.

Pamoja na kuwepo kwa mafanikio ya kuudhibiti moto huo, lakini upepo mkali unafanya kazi ya kuuzima kuwa ngumu zaidi, Idara ya Tiba na Uchunguzi ya Kaunti ya Los Angelese inasema.

Wanasayansi wanasema mioto ya nyika katika Jimbo la California inasababishwa na mabadiliko ya tabianchi na jimbo hilo linaongoza kuwa la pakee katika matukio hayo katika historia yake.

Eneo lote lililoteketezwa na mioto ya Palisades, Eaton na Hurst ni ekari za mraba 38,629, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Shirika la Cal Fire.

Eneo hilo lililotekezwa la ukubwa maili za mraba 60 ni kubwa zaidi ya eneo wa jiji la Paris ufaransa, lenye ukubwa wa maili za mraba 40.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages