
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
-------------------------------------
Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye aliteuliwa na Mkutano Mkuu wa chama hicho Januari 19, 2025 kugombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, atatambulishwa rasmi kesho jijini Dodoma.
Taarifa iliyotolewa na Idara ya CCM ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo jijini Dodoma jana, ilisema hafla ya utambulisho huo itahudhuriwa na viongozi mbalimbali, wanachama na wakereketwa wa chama hicho tawala.
Mkutano Mkuu Maalum wa CCM pia ulimteua Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt Emmanuel Nchimbi kuwa Makamu wa Rais na mgombea mwenza wa Rais Samia katika uchaguzi mkuu ujao.
Chama hicho kikongwe barani Afrika kitakuwa na shamrashamra kubwa katika utambulisho huo kwa sababu pia kitakuwa kikisherehekea miaka 48 tangu kuanzishwa kwake kufuatia muungano wa vyama vilivyopigania uhuru, TANU na Afro-Shiraz mwaka 1977.
Rais Samia ambaye ni mwanamke wa kwanza Tanzania kushika kushika wadhifa huo anasifika kwa kuimarisha uchumi, kuheshimu ushindani wa kisiasa na kuleta mageuzi katika utawala wa sharia.
Wachambuzi wa siasa wanatabiri kwamba Rais Samia atajizolea kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu ujao kutokana na uthubutu wake wa kubadili sura ya Tanzania kiuchumi, kisiasa na kiutawala kwa kuzingatia mambo ya msingi waliyofanya watangulizi wake.
Chama Cha Mapinduzi ambacho anakiongoza Rais Samia kama Mwenyekiti wake, bado kinazingatia siasa ya kujitegemea kwa kutumia amali na ujuzi wa Watanzania kujiletea maendeleo katika zama hizi za utandawazi duniani.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>Aga Khan IV afariki dunia nchini Ureno
>>Tarime Mji wapitisha bajeti ya bilioni 30.851/-, DC Gowele asisitiza usafi Hospitali ya Wilaya
>>M23 yatangaza kusitisha mapigano DRC kwa sababu za kibinadamu
>>Mkutano Mkuu WAMACU wapitisha ununuzi kiwanda cha chai, RC awapongeza kwa kuitangaza kahawa ya Tarime
No comments:
Post a Comment