NEWS

Thursday, 13 February 2025

Sekondari ya Nyamongo na nyingine 4 zapokea msaada wa vitabu kutoka Taasisi ya Nyambari Nyangwine



Mwakilishi wa Nyambari Nyangwine Foundation, Sospeter Migera Paul (wa tatu kutoka kushoto) akikabidhi msaada wa vitabu katika Shule ya Sekondari Ingwe jana Februari 12, 2025.
-----------------------------------------

Na Godfrey Marwa, Tarime

Nyambari Nyangwine Foundation (NNF) imeendelea kusambaza msaada wa vitabu vya kiada na ziada kwenye shule za sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini), ambapo jana Februari 12, 2025 ilizifikia sekondari tano katika tarafa ya Ingwe.

Sekondari hizo ni Ingwe, Nyamongo, Matongo, Kemambo na Nyabichune zilizopo jirani na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara.


Makabidhiano ya msaada wa vitabu katika Shule ya Sekondari Nyamongo.
----------------------------------------


Makabidhiano ya msaada wa vitabu katika Shule ya Sekondari Kemambo.
--------------------------------------

Akizungumza baada ya Mwakilishi wa NNF, Sospeter Migera Paul kukabidhi msaada huo wa vitabu, mkazi wa mji wa Nyamongo, Julius Mang'eng'i aliishukuru taasisi hiyo na kuwahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii.

"Tumieni msaada huu kusoma kwa bidii, tunataka Nyambari mwingine atoke humu humu. Msaada huu utatunyanyua kwenda mbali, huyu anafahamika ni mchangiaji wa maendeleo siku nyingi, anaweza kutusaidia zaidi," alisema Mang'eng'i.


Makabidhiano ya msaada wa vitabu katika Shule ya Sekondari Matongo.
--------------------------------------

Nao walimu na wanafunzi wa shule ya Sekondari Ingwe waliishukuru Taasisi ya Nyambari Nyangwine kwa msaada huo wa vitabu na kuahidi kuleta matokeo bora, huku wakitaja ukosefu wa vitabu vya Tamthiliya na Riwaya kama kama tatizo kubwa kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita.

Msaada wa vitabu unaosambazwa na Nyambari Nyangwine Foundation inatoa msaada huo wa vitabu kuunga juhudi za serikali kwenye uwekezaji na uboreshaji wa elimu nchini.

Makabidhiano ya msaada wa vitabu katika Shule ya Sekondari Nyabichune. (Picha zote na Mara Online News)
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages