NEWS

Thursday, 13 February 2025

Tarime: Heche kuchinja ng’ombe 20 kujipongeza kwa ushindi CHADEMA



Na Joseph Maunya, Tarime

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa (Bara), John Heche (pichani katikati) amewaalika wananchi kuhudhuria sherehe yake ya kujipongeza na kushukuru kwa ushindi wa nafasi hiyo.

Akizungumza jana Jumatano baada ya kuwasili na kupokewa na wananchi katika mji wa Tarime mkoani Mara, Heche alisema ng’ombe 20 watachinjwa katika sherehe hiyo itakayofanyika kijijini kwake Kitagasembe.

Kabla ya kufikaTarime kiongozi huyo wa CHADEMA alifanya mikutano mingine ya hadhara katika maeneo ya Lamadi, mkoani Simiyu na Bunda mkoani Mara.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages