Na mwandishi wetu, Serengeti
Jumla ya wanafunzi 360
wa darasa la tano kutoka shule mbalimbali za msingi katika Wilaya za Serengeti
na Bunda wameshirki katika kambi la kingereza ambalo huandaliwa na Grumeti Fund
wakati wa likizo.
Kambi hizo zilifanyika katika vituo vitatu ambavyo ni kituo cha elimu ya mazingira cha
Grumeti Fund, Mugumu na Bunda.
Kila kambi lilifanyika kwa siku sita kwa lengo
la kuwajengea wanafunzi hao uwezo wa kujiamini, kupenda na kuwa na uwezo wa kujifunza kingereza.
Walimu ambao ni
wabobezi wa lugha kutoka chuo cha Concordia kilichopo Marekani
wakisadiana na walimu wa Tanzania kutoka shule husika walishiriki kutoa mafunzo
hayo kwa wanafunzi hao kwa njia mbalimbali kama vile nyimbo, kuchora, hadithi na michezo.
Kwa kufanya hivyo
wanafunzi walengwa wataweza kumudu hata
masomo mengine ambayo yanafundishwa kwa lugha ya kingereza mara watakapojiunga na elimu ya sekondari,.
Hadi sasa wanafunzi 690
wamenufaika na mpango huo tangu mwaka 2017 ulipoanzishwa na Grumeti Fund ikiwa
ni sehemu ya huduma na maendeleo za
jamii inayotoa kuchangia kuinua ubora wa sekta ya elimu katika vijiji 21
ambavyo vinapakana na mapori tengefu ya Ikorongo/Grumeti.
No comments:
Post a Comment