NEWS

Wednesday 10 July 2019

BEST NASSO AAHIDI KUINUA VIJANA WENYE VIPAJI VYA KUIMBA TARIME

Na mwandishi wetu 

BEST NASSO AAHIDI KUINUA VIJANA WENYE  VIPAJI VYA KUIMBA TARIME






Msanii maarufu wa bongo flava Hamis Nassoro maarufu kama Best Nasso amewaasa  vijana kujituma na kuwa mstari wa mbele katika kuchangamkia fursa zinazojitokeza ili kuinua vipaji vyao suala ambalo litawasaidia vijana kuondokana  umaskini ikiwa ni pamoja na kujipatia ajira na kuzidi  kupata maendeleo binafsi na nchi kiujumla


Akiongea na wananchi kwenye sherehe ya kufunga ligi ya mpira wa miguu ( RICH CUP )  katika kata ya Magoma iliyokpo wilayani Tarime mkoani  Mara msanii  huyo amesema kuwa  amefurahi kufika katika sherehe hiyo na kuona wananchi wa eneo hilo wakipenda sana michezo kwa kushangilia ushindi uliopatikana baada ya mechi hizo 

Best Nassso ameendelea kusema kuwa  anampongeza mfadhili wa michezo hiyo Bwana Richard Matiko kwa kuanzisha ligi hiyo na kumuomba kuendelea na moyo wa hivyo kwani kwa kufanya hivyo ataweza kuibua vipaji mbalimbali vya vijana huku akionyesha kuguswa na jambo hilo nakuwaasa wadau wengine ambao  wana uwezo wa kufanya hivyo kuhakikisha wanajikita katika kufanya maendeleo jambo ambalo litasaidia kubadili maisha ya waliowengi huku akihaidi kusaidia huduma ya kurekodi miziki kwa wasanii wa nyumbani watakao onyesha kuwa na nia ikiwa ni pamoja na kufanya vizuri katika uimbaji.

Aidha mfadhili wa michezo hiyo bwana Richard Matiko amesema kuwa ameamua kufanya hivyo ili kukuza vipaji vya vijana  huku akitaja mikakati aliyonayo ikiwa ni kuanzisha ligi katika kata zote za  Tarime mjini  pamoja na kuelekeza nguvu pia katika kukuza vijana wa kike baada ya kuwa ligi hii ya mpira wa miguu kwa wavulana kumalizika

Hata hivyo Afsa mtendaji wa kata ya Magoma Peter Patroba ameweza kutoa shukrani za dhati kwa mfadhili  huyo nakuomba kuendelea kufanya hivyo jambo ambalo linasaidia kupunguza tabia zisizokuwa nzuri katika jamii kwani michezo ni ajira ukiondolea mbali faida nyinginezo kama kuburudisha na kujenga mwili.

Katika  ligi hiyo ambayo imejumuisha timu kama vile Nyasaricho,Nyamwigula,Magoma Fc ,yuleka Naymisecho mshindi wa kwanza namesocho  ameweza kuibuka na kiasi cha shilingi milioni mbili ,mshindi wa pili  nyansaricho milioni moja na mshindhi wa tatu ambaye ni Yuleka  ambapo makaptaini wa timu zote mbili wamesema kuwa mchezo huo ulikuwa huru na haki wenye upendo mkubwa bila kujali matokeo yaliyopatikana.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages