Na Mwandishi Wetu ,Musoma
Dereva wa gari la Mkuu wa Mkoa wa Mara na mtoto wake wako chini ya mikono ya jeshi la
polisi baada kijana wa dereva huyo
kuchukua gari la serikali analotumia Mkuu wa Mkoa na kisha kupata ajali jana Jumapili.
Hata hivyo dereva huyo wa Mkuu wa Mkoa alipoteza
fahamu baada ya tukio hilo kutokea na
kulazwa katika hospitali ya Mkoa wa Mara mjini Musoma.
Kijana wa dereva huyo pia
alilazwa katika hospitali hiyo ya Mkoa wa Mara baada ya kupata majeraha
katika ajali hiyo .
“ Hali zao zinaendelea vizuri na wako hospitalini
chini ya ulinzi mkali wa polisi” Kamanda wa Polisi Mkoa(RPC) wa Mara Juma Ndaki
ameimbia Mara Online News leo mchana.
Kamanda Ndaki hakupenda kutaja majina yao kwa sasa.
No comments:
Post a Comment