NEWS

Monday 5 August 2019

SEKTA YA MADINI TARIME SASA KUPAA , NI BAADA YA JUHUDI ZA DC KABEHO KUANZISHA MASOKO YA MADINI NYAMONGO NA TARIME MJINI KUPATA BARAKA YA WIZARA





Na Clonel Mwegendao

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ametoa baraka kwa Wilaya ya Tarime kufungua masoko mawili ya kuuza madini ya dhahabu katika eneo la Nyamongo na Tarime Mjini .

 Naibu Waziri Nyongo ametaka  masoko hayo kuanza kufanya kazi kesho Julai 6.
   
“ Naomba kusema rasmi kuanzia tarehe 6 masoko ya Nyamongo na Tarime yafunguliwe rasmi , hakuna mjadala wa hilo”, Nyongo alisisitiza  wakati akiongea na wachimbaji wadogo na wadau wengine wa sekta  ya madini katika chuo cha Ualimu Tarime  jana jumapili.

Mkuu wa Wilaya ya Tarime(DC) Charles Kabeho amesema kufunguliwa kwa masoko hayo kutasogeza huduma  karibu kwa wachimbaji wa dhahabu wa Nyamongo  na  Mji wa Tarime .

Hatua hiyo pia inatarajiwa kupunguza utoroshwaji wa dhahabu kwenda nchi jirani kwa njia ya magendo.

“ Natambua soko la  madini ya dhahabu  lipo Musoma lakini  na nia yetu ni kusogeza huduma  kwa wachimbaji . Kuna baadhi ya watu wakitoka tu  kwenye mashimo wanahitaji fedha ya dharula na kusafiri kwenda Musoma wanaona ni mbali“, alisema Kabeho .

TAZAMA VIDEO 


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages