NEWS

Saturday 3 August 2019

DIWANI SERENGETI: TUNA SHIDA KUBWA YA MAJI


Diwani Kata ya Kenyamonta  Sosteness Samwel
Wananchi wa kata ya Kenyamonta Wilayani Serengeti wanakabiliwa na uhapa wa maji safi na salama baada ya mashine iliyokuwa inatumika kusukuma maji kuharibika.
Diwani wa kata hiyo Sostenes Samwel amesema wananchi wa kata yake sasa wanatumiwa maji maji ya bwawa ambayo sio safi na salama.
‘’Kwakweli tatizo la maji sasa limegeuka kuwa ker okubwa kwa wananchi wa kata ya Kenyamonta. Naiomba serikali na wadau wengine wa maendeleo watusadie ili wananchi wapate maji safi na salama”, Samwel  ameambia Mara Online News leo .
Amesema maeneo mengi ya kata hiyo hayana miundombinu ya maji .
Hata hivyo diwani huyo ametoa wito kwa wananchi wa kata hiyo kuendelea kuchemsha maji ya kunywa wakati juhudi zikutatua tatizo la maji zinaendelea katika  kata hiyo.
.
(Na Clonel Mwegendao, Serengeti)


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages