NEWS

Monday, 20 July 2026

Miradi mipya ya CSR Barrick North Mara yaendelea kukamilika



Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Matera Newland Chacha, akizungumza katika moja ya hafla za makabidhiano ya miradi mipya ya CSR Barrick North Mara.

Na Mwandishi Wetu
Tarime
-------------

Halmashauri ya Wilaya ya Tarime inaendelea kupokea miradi mipya ya maendeleo iliyotekelezwa na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara chini ya mpango wa Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR).

“Tayari tumepokea miradi mipya ya CSR kwenye sekta mbalimbali, na tunawashukuru wakandarasi ambao wamekamilisha miradi yao kwa wakati,” Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Matera Newland Chacha, aliliambia Gazeti la Sauti ya Mara jana.

Matera alisema miradi iliyokamilika na kupokekewa ipo kweye sekta za elimu, afya na barabara.

“Mfano, tumekepokea nyumba za walimu, vyumba vya madarasa, madawati, barabara, zahanati na nyumba za watumishi wa afya,” Matera ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Manga kupitia chama tawala - CCM,” alisema.

Mgodi huo wa North Mara unatarajia kukamilisha miradi mipya ya CSR 103 inayotekelezwa katika halmashauri hiyo wakati wowote kuanzia sasa.

Hadi Mei mwaka huu, miradi 70 kati ya hiyo ilikuwa imekamilika kwa asilimia 100, huku 33 ilikuwa kwenye hatua za mwisho, kwa mujibu wa ripoti ya mgodi huo.

Miradi hiyo inatekelezwa katika maeneo mbalimbali ya halmshauri hiyo yeye utajiri mkubwa wa madini.

Tatwimu zinaonesha, mgodi huo ambao unaendeshwa na Kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals, umetoa shilingi bilioni 26 kuanzia mwaka 2019 hadi 2025 kwa ajili ya utekeleza miradi mbalimbali ya kijamii kupitia mpango wa CSR.

Wakati huo huo, kwa mara ya kwanza, mgodi huo utaeleleza sehemu ya mamilioni ya fedha za CSR kwenye utekelezaji wa miradi ya kimkakati katika vijiji vilivyopo jirani.

Miradi hiyo ni ujenzi wa jengo la soko la dhahabu katika mji mdogo wa Nyamongo na ujenzi wa kituo cha mabasi katika eneo la Nyamwaga yalipo makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.

Chanzo: Gazeti la Sauti ya Mara

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages