Ushirikiano mzuri kati ya Serikali ya Tanzania na Taasisi ya Grumeti Fund umefanikisha kuhamisha faru weusi tisa kutoka Afrika Kusini kuja Serengeti.
Faru hao wamewasili salama leo(Jumanne) asubuhi kwa ndege kubwa ya mizigo katika maeneo ya hifadhi ya Grumeti .
Mkuu wa Mkoa wa Mara(RC) Adam Malima ameongoza hafla ya mapokezi ya faru hao.
“ Tunataka afaru
waongezeke Serengeti na tusijekujaribishana kwa hili”, Mkuu wa Mkoa alionya
mara baada ya kupokea faru hao.
Wajumbe wa
kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa wa Mara na Wilaya ya Serengeti walihudhuria
mapokezi ya faru hao.
Hafla hiyo pia ilihudhuhuriwa na wahifadhi
wa wanyamapori kutoka taasisi mbalimbali za serikali na Grumeti Fund.
“ Tumepokea
faru hawa na tunawapeleka mbugani hili ni jukumu kubwa na ndio maana hata mapokezi yake sio kitu
kidogo”, alisema RC Malima.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alishukuru serikali ya
Tanzania na taaisi ya Grumeti Fund kwa kufanikisha kuwaleta faru hao Serengeti.
Grumeti Fund ni taasisi inayojihusisha na uhifadhi
wa wanyamapori na maendeleo ya jamii katika mapori tengefu ya Ikorongo-
Grumeti.
Mkurugenzi Mtendaji wa Grumeti Fund Stephen Cunliffe
alisema ushirikiano mzuri kati ya Serikali ya Tanzania na taasisi ya Grumeti
Fund umefanikisha kuhamisha faru hao
weusi kutoka Afrika Kusini kuja
Serengeti.
Cunliffe alisema taasisi hiyo itaendelea kuunga
mkono juhudi za kuongeza faru weusi katika ikolojia ya Serengeti.
Safi saana siku moja Serengeti itakuwa kivutio bora dunian zaid ya sasa
ReplyDelete