Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima leo amezindua maadhimisho ya siku
ya Mara 2019 katika viwanja vya sokoine
mjini Mugumu , Wilayani Serengeti.
RC Malima amesema maadhimisho ya siku ya Mara ni muhmu katika uhifadhi endelevu wa bonde la
Mto Mara.
Mkuu wa
Wilaya ya Serengeti Nurdin Babu amewetaka
wananchi wa Serengeti kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maadhimisho hayo ambayo yatahitimishwa Septemba 15.
Kaimu Mkurugenzi wa
wa miundombinu ya uchumi na huduma za jamii kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Eliabi Khalid amesema utunzaji wa mazingira ya bonde la mto Mara hauwezi kufanikiwa bila ushirikiano mzuri baina ya Tanzania na
Kenya .
Mataifa ya Tanzania na Kenya huadhimisha siku ya
Mara Septemba 15 kila mwaka .
Maadimisho hayo hufanyika kwa kupokezana ambapo mwaka
huu Tanzania ndiye itakuwa mwenyeji wa
sherehe hizo za siku ya Mara .
Kauli mbiu ya madhimsiho hayo mwaka huu ni:
“,Mimi
mto Mara , Nitunze Nikutunze”.
No comments:
Post a Comment