Kamisheni
ya bonde la ziwa Victoria(LVBC) imezindua  wimbo wa Mara ambao 
unahamsisha utunzaji wa  mazingira  ya  bonde la
 Mara  kwa upande wa Kenya na Tanzania .
Katibu
Mtendaji wa LVBC  Dkt Ali –Saidi Matano alizindua wimbo huo  Jumapili iliyopita  mara tu baada ya kilele cha maadhimisho ya
nane ya siku ya Mara katika viwanja vya Sokine Mjini Mugumu Jana.
 
“ Wimbo huu umekuja kwa wakati mwafaka na  tunaomba uimbwe kwenye redio,
runinga, madukani na hata kwenye  mito wakati akina mama wanachota maji,
na wafugaji wakati wakiwa kwenye malisho ya mifugo yao nan a wanafunzi
mashuleni””,  Dkt Matano alisema.
Dkt
Matano alishukuru shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira  na
Wanyamapori(WWF) kwa kuja na wazo la kutumia njia ya wimbo katika kuelimisha
jamii kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mto Mara .
.Wimbo
huo unamzungumzia  mama akiwa kwenye shida analia akihataji msaada na mama
huyo ni mto Mara ,  alisema William Ojwang kutoka WWF Kenya . 
“
Tunataka wimbo huu utumike kuendeleza kampeni ya kuhifadhi mto Mara na wimbo
huu uendelee kutukumbusha kuwa mama yetu(mto Mara) analia na anahitaji
msaada”,alisema Ojwang.  
          
 
 
 
 
 
 
.jpeg) 
No comments:
Post a Comment