Mshambuliaji wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Ureno, Christiano Ronaldo
jana usiku ameweka rekodi ya kuwa mchezaji
wa tano wa muda wote duniani kufikisha magoli
700.
Goli la 700 la Christiano Ronaldo limefungwa
usiku wa kuamkia leo Jumanne Oktoba 15, 2019 dhidi ya Ukraine kwenye mchezo wa kufuzu michuano ya Euro.
Kwa rekodi hiyo , Ronaldo anakuwa mchezaji
wa 5 kufikisha magoli 700 akiwa nyuma ya Pele mwenye magoli 757, Josef
Bicangoli 756, Romario goli 749, FerencPuscas 704.
Na klabu alizotupia magoli hayo ni Sporting Lisbon 5 ,
Manchester United 118, Real Madrid 450, Juventus 32 na Ureno magoli 95
Kwa sasa Ronaldo amebakisha magoli 57
kuvunja rekodi iliyodumu muda mrefu mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil,
Pele ya magoli 757
No comments:
Post a Comment