NEWS

Wednesday 27 November 2019

MJUMBE WA MKUTANO MKUU CCM TAIFA AING'ARISHA OFISI YA CCM



Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) taifa ndugu  Gerald Martine leo ametoa bango la kisasa na alama elekezi  ili kusadia kutambulisha ofisi za CCM  Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.


Msaada huo umepokelewa na Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime ndugu MKaruka kura.



 Ndugu Martini ambaye ni kada wa miaka mingi wa CCM amasema ametoa msaada huo ili kuboresha huduma zinazotolewa na chama hicho kwa wanachama wake na wananchi  kwa ujumla.



Akiongea baada ya kupokea msaada huo  Katibu wa CCM Wilaya yaTarime Ndg Hamisi Mkaruka Kura  amesema uwepo wa bango hilo na alama elekezi  vitasadia kuboresha  huduma kwa wanachama wa CCM na  wananchi .

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages