Daraja la zamani la Mto Mara ambalo linalouganisha
Wilaya za Serengeti na Tarime limesombwa na maji na nyumba kadhaa kujaa maji lakini mawasiliano kati ya wilaya hizo hayatakatika kwa sababu
tayari serikali imeishajenga daraja jipya la kisasa kwa
gharama ya zaidi ya bilioni nane katika eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti(DC) Nurdin Babu alifika
jana Alhamisi katika eneo la tukio mara tu baada ya kupata taarifa kuwa daraja hilo
limesombwa na maji na kuwataka wananchi waliojirani kuhama eneo hilo mara moja baada ya nyumba zao pia kujaa maji .
Abiria wakiangalia jinsi daraja la zamani lamto Mara limesombwa na maji |
Hata hivyo wananchi walipongeza serikali kwa kujenga
daraja jipya ambalo limenusuru mawasiliano kati wilaya za Tarime na Serengeti
kukatika..
Viongozi wa mkoa wa Mara wakiwa katika eneo la daraja jipya la mto Mara hivi karibuni |
Daraja hilo jipya limejengwa taa kubwa huku sehemu
ya barabara yae upande waTarime na Serengeti ikijenwa kwa kiwano cha lami
( Habari na Mwandishi Wetu, Mugumu)
No comments:
Post a Comment