Mbunge
wa Jimbo la Musoma Vijijini katika mkoa wa Mara, Profesa Sospeter Muhongo,
ametumia zaidi ya milioni 10 kuchagia ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Wilaya ya Musoma Vijijini katika kijiji cha Murangi.
Pamoja
na shughuli nyingine, fedha hizo zimetumika kugharimia ufyatuaji na umwagiliaji
matofali (Sh milioni moja), ununuzi wa saruji mifuko 200 (Sh milioni nne) na
malipo ya fundi (Sh milioni nne).
No comments:
Post a Comment