NEWS

Tuesday 7 April 2020

Watu 18 wanusurika kufa ajali ya basi Simiyu


WATU 18 wamenusurika kufa baada ya basi dogo lenye namba T 565 DKV la Kampuni ya Magumba Express walilokuwa wakisafaria kutoka Bariadi mkoani Simiyu kwenda Nzega mkoani Tabora kuacha njia na kupindukia mtaroni wakati likijaribu kulipita gari lenye namba T 933 EKQ aina ya Toyota Mark 11.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Deusdedit Mataba amethibitisha ajali hiyo akisema imetokea Jumatatu April 6, 2020 saa 2:35 asubuhi katika kijiji cha Ng’hami wilayani Maswa, Simiyu.
 Kwa mujibu wa Kamanda Mataba, majeruhi hao wamepelekwa kutibiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Maswa na kwamba jeshi hilo linamsaka dereva wa basi aliyetoroka baada ya ajali hiyo kwa ajili ya kujibu mashtaka yanayomkabili likiwamo la kuendesha kwa mwendo kasi.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dkt Bwire Robert amekiri kupokea majeruhi hao (wanaume 15 na wanawake watatu) Jumatatu saa 3:00 asubuhi na amesema hali za wengi wao zinaendelea kuimarika isipokuwa mmoja anayepelekwa Hospitali ya Rufaa Bugando mkoani Mwanza kwa ajili ya matibabu ya kibingwa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages