Virusi hivi vinaweza kusababisha magonjwa kwa wanyama na
binadamu. Kwa binadamu, virusi mbalimbali vya Corona vinajulikana kusababisha
maambukizi kwa njia za hewa ikiwemo mafua ya kawaida, MERS na SARs.
Tafiti nyingi zinaendelea kote duniani
na mengi bado yanaendelea kugundulika kuhusu kirusi hiki kipya, lakini mpaka
sasa sayansi inatuambia kirusi hiki kinaambukizwa kutoka kwa binadamu mwenye
maambuki kwenda kwa mwingine kupitia matone madodo madogo kutoka puani au
mdomoni pale mtu mwenye maambukizi ya corona anapopiga chafya, kukohoa au
kuongea.
Matone haya ni mazito, hivyo hushindwa kusafiri mbali. Pia
yanaweza kudondokea kwenye vitu na sehemu kama meza na kitasa.
Kupitia tafiti, imegundulika kwamba virusi vya corona
winaweza kuishi mpaka saa 72 kwenye plastiki na chuma kisichoshika kutu, chini
ya saa 24 kwenye mbao na chini ya saa nne kwenye bati.
Mtu anaweza kuambukizwa corona iwapo atakuwa karibu na mtu
mwenye virusi hivyo au akishika sehemu ambazo matone yenye virusi yamedondokea.
Ugonjwa
huathiri umri na rika zote, ingawa watu wenye umri mkubwa/wazee, wale wenye
magonjwa sugu kama pumu, kisukari, presha ya juu, magonjwa ya figo, matatizo ya
mapafu au wenye saratani wana hatari kubwa zaidi ya kupata ugonjwa wa COVID-19
na unaweza kusabaisha kifo.
Kila
mtu kwenye jamii ana wajibu wa kuchukua hatua na kujilinda.
Dalili
za ugonjwa wa Corona ni pamoja na homa kali, kikohozi kikavu na kuchoka.
Wagonjwa wengine hupata mafua, maumivu yakichwa, mwili na kuharisha.
Inachukua
kati ya siku mbili mpaka 14 kwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa wa corona kuonesha
dalili yeyote kati ya hizi zilizotajwa.
Mpaka
asilimia 80 ya watu wanaopata corona wanakuwa na dalili ndogo au hawana dalili
kabisa, asilimia 15 wana dalili za kati na asilimia tano wanakuwa na dalili
kali ikiwepo shida kubwa ya kupumua mpaka kuhitaji huduma za wagonjwa mahututi
(ICU) na msaada wa kupumua kupitia mashine ambazo kitaalamu zinaitwa ventilators.
Mashine zinazotoa msaada wa kupumua kwa wagonjwa (Ventilators) (Picha kwa msaada wa mtandao) |
Ni
muhimu kuzingatia kwamba, haijalishi ufinyu wa dalili, mtu yeyote mwenye maambukizi
ya corona hata kama hana dalali ana uwezo wa kuambukiza wengine.
Pindi
utakaposikia dalili hizi tafuta msaada wa haraka kwenye hospitali iliyopo
karibu yako ama piga 199 kupata ushauri wa kitabibu zaidi.
Virusi
vya corona mwilini hushambulia mfumo wa hewa, hasa vifuko vidogo vidogo
vilivyoko kwenye mapafu viitwavyo alveoli ambavyo kazi yake kubwa ni
kusafirisha damu na kuhakikisha inakuwa na oksijeni ya kutosha.
Hata
bila kuumwa, unavyotoa hewa ndani, alveoli zinajaa oksjeni na inapeleka
hiyo oksijeni kwenye damu na unapotoa hewa nje, alveoli zinajikunja na
zinatoa hewa ya kaboni dayoksaidi.
Vifuko
hivi vinaathirika pale mtu anapopata virusi vya corona, uwezo wa mapafu
kuhakikisha oksijeni inaingia kwenye damu na kaboni dayoksaidi inatolewa nje
unapungua.
Mgonjwa
huanza kuhisi hewani finyu na mwili kufanya kazi ya ziada kuvuta hewa kwa nguvu
zaidi, hii ndio shida kubwa inayowakumba wagonjwa wa corona na kwa wengine
mpaka kusababisha kifo.
Lakini
taarifa za kisayansi zinaonesha kwamba, kuna watu ambao wanapungukiwa oksijeni
mwilini lakini hawaoneshi dalili zozote kitaalamu wanaitwa “Silent Hypoxia” na
hili ndilo kundi la hatari maana wanakufa kimya bila kujitambua.
Mpaka
sasa, corona haina dawa wala chanjo, kilichopo ni kinga tu.
Katika
kujikinga, Shirika la Afya Duniani (WHO) linashauri kuhakikisha tunaweka umbali
wa kiasi cha mita moja mpaka tatu kati ya mtu na mtu, ili mtu akiongea,
akikohoa au akipiga chafya matone yenye virusi hayamkuti aliye karibu naye.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dr. Tedros Adhanom Ghebreyesus (Picha kwa msaada wa mtandao) |
Tatu,
osha mikono na maji yanayotirirka na sabuni mara kwa mara na jiepushe
kugusagusa uso wako mara kwa mara kwa mikono.
Nne,
kupunguza mizunguko isiyo na lazima, rudi nyumbani baada ya kazi, epuka maeneo
ya misongomano.
Tano,
tumia vyakula vya kuimarisha kinga ya mwili ikiwepo matunda na mboga za majani
zenye vitamini C kwa wingi ikiwepo brokoli, hoho nyekundu, machungwa, malimau.
Ningependa
kufafanua kitaalamu umuhimu wa kuosha mikono kwa maji yanayotirika. Hii ni njia
madhubuti sana ya kujikinga na gonjwa la corona.
Kirusi
cha corona kimetengenezwa na vinasaba ambavyo vimefungwa kwenye ukuta wa
mafuta. Sabuni, inaharibu huu ukuta wa mafuta na kufanya kirusi kibomoke na
kisiwe na madhara tena.
Picha ikionyesha namna ya kunawa mikono kwa maji yanayotiririka (Picha kwa msaada wa mtandao) |
Unaponawa mikono na maji yanayotiririka vile virusi vilivyokufa
vinatoka kabisa mikononi mwako, na hii ni sababu inayofanya kunawa mikono na
maji yanayotirika kuwa njia bora zaidi ya kuhakikisha usafi na usalama wa
mikono yako kuliko hata kutumia kipukusi (hand sanitizer).
Unapotumia kipukusi, ingawa virusi vinakufa lakini vinabaki
mikononi mwako mpaka pale utakapoosha mikono yako.
Nitoe rai, tuenendelee kujikinga na kufuata masharti na maelekezo
yote yanayotolewa na wataalamu wa afya na mamlaka za afya za serikali.
Na Daktari Shally Zumba Mwashemele
Simu: +255 716 615651 Barua Pepe: shallyzumba@gmail.com
No comments:
Post a Comment