NEWS

Monday 4 May 2020

Muhongo, wadau waboresha shule Musoma Vijijini



SHULE ya Msingi Murunyigo iliyopo kijiji cha Kiemba, kata ya Ifulifu, jimbo la Musoma Vijijini, imeboreshewa miundombinu kutokana na michango mbalimbali ya wananchi, mbunge, serikali na wadau wa maendeleo.

Wadau wa maendeleo walioshirikiana na Mbunge wa Jimbo, Profesa Sospeter Muhongo, serikali na wanakijiji katika kuboresha miundombinu ya shule hiyo iliyoanza mwaka 1956 ni Shirika la PCI na Benki ya CRDB.

Msaidizi wa Mbunge, Fedson Masawa, ameiambia Mara Online News leo Mei 4, 2020 kwamba Benki ya CRDB imechangia vifaa mbalimbali vya kukamilisha ujenzi wa chumba cha darasa katika shule hiyo.

Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kiemba, Regina Chirambo, ametaja vifaa vilivyotolewa na benki hiyo kuwa ni saruji mifuko 60, rangi ndoo mbili na kopo moja, square pipe tano, flat bar 10, komeo na bawaba.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji, Rocket Rukiko, amesema Shirika la PCI limejenga vyoo na kutoa chakula na vitabu kwa wanafunzi na elimu ya afya katika shule hiyo ya Murunyigo.
Wakazi wa kijiji ch Kiemba wakishiriki katika uboreshaji wa miundombinu ya Shule ya Msingi Murunyigo.
Kwa upande wake, Mbunge Profesa Muhongo, amechangia uboreshaji wa miundombinu ya shule hiyo kwa kutoka saruji mifuko 60, madawati 106 na vitabu mbalimbali kwa ajili ya maktaba ya shule hiyo.


Mbunge huyo amesema serikali kupitia mradi wake wa Equit inaendelea kushirikiana na wananchi katika kuboresha zaidi mazingira ya elimu shuleni hapo.

Profesa Muhongo, viongozi na wanakijiji wamewashukuru wadau wa maendeleo waliochangia uboreshaji wa miundombinu ya shule hiyo na kutoa mwito kwa wengine kujitokeza kuwaunga mkono katika juhudi hizo.


(Habari na Christopher Gamaina,)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages