NEWS

Wednesday 3 June 2020

CHAVITA Simiyu wapewa mabango kuelimisha kuhusu Corona

CHAMA cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) chenye makao makuu jijini Dar es salaam kimetoa mabango 41 yenye jumbe mbalimbali kwa wanachama wake mkoani Simiyu, kwa ufadhili wa taasisi ya The Foundation for Civil Society (FCS).
Afisa Ustawi wa Jamii Simiyu, Daniel Mapunda (kushoto), akimkabidhi bango Mwenyekiti wa CHAVITA Simiyu, Mhandi Zephania. Kulia ni Katibu wa CHAVITA Simiyu, Alex Benson

Akipokea mabango hayo mjini Bariadi leo Juni 3, 2020, Katibu wa CHAVITA Simiyu, Alex Benson, amesema yatatumika kuelimisha viziwi na jamii kwa jumla namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona (covid 19).

Aidha, chama hicho kimependekeza mabango hayo yabandikwe kwenye maeneo mbalimbali kama vile hospitali, vituo vya polisi, masoko na sehemu za kazi za watu wenye ulemavu huo.
Afisa Ustawi wa Jamii Simiyu, Salama Rajabu (mwenye blauzi), akimkabidhi bango Katibu wa CHAVITA Simiyu, Alex Benson
Hata hivyo, Benson amesema mabango hayo hayakidhi mahitaji ya mkoa wa Simiyu na kuomba elimu itolewe moja kwa moja sambamba na vifaa kinga kwa viziwi.


Katibu huyo wa CHAVITA amesema uwepo wa wakalimani wa lugha ya alama katika vituo vya afya utarahisisha mawasiliano kati ya viziwi na watoa huduma. 

(Imeandikwa na Anita Balingilaki, Bariadi)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages