NEWS

Saturday 13 June 2020

DC Tarime aongoza mamia kuaga mwili wa Mwalimu Happy


Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhandisi Mtemi Msafiri(pichani katikati), leo Juni 13, 2020 ameongoza mamia ya wananchi mjini Tarime kuaga mwili wa Malimu Happy Munisi aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza alikokuwa akipata matibabu baada ya kupata ajali ya moto ambayo pia ilisababisha kifo cha mume wake, Mwalimu Richard Leonce, Jumatano iliyopita.
DC Msafiri akitoa salaam za pole 

Katika salamu zake za pole, DC Msafiri amesema Serikali inaendelea kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Baba mkwe wake marehemu Mwalimu Happy (wakwanza kulia) akishiriki katika ibaada ya kuaga mwili
Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda mkoani Manyara ambapo mazishi yake na mwenzi wake huyo  yamepangwa kufanyika kwa pamoja.
Masister wakiwa katika ibaada ya kuaga mwili wa marehemu
Hadi mauti yanawafika, Richard alikuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Azimio iliyopo Tarime Mjini na mke wake, Happy, alikuwa akifundisha katika Shule ya Msingi Remagwe iliopo Tarime Vijijini.

Baadhi ya wananchi  baada ya kuaga mwili wa mpendwa wao
Mkurugenzi na wafanyakazi wa Mara Online News wanatoa pole kwa ndugu, jamaa, walimu, marafiki na wananchi wote wa Tarime kutokana na msiba huo mzito

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages