NEWS

Sunday 14 June 2020

Katibu wa AMCOS Simiyu kizimbani kwa uhujumu uchumi



TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, imemfikisha mahakamani Katibu wa AMCOS ya Mwanga kituo cha Nangale, Masanja Mabula kwa uhujumu uchumi.

Mabula amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Simiyu, mbele ya Hakimi Mkazi Mfawidhi, Venance Mlingi, akishitakiwakwa kughushi shilingi milioni 7, wizi wa shilingi milioni 12 na kusaibabisha mamlaka hasara ya shilingi milioni 22.5.
Kupitia kesi namba 23/2020, Mabula amesomewa mashitaka hayo juzi na Mwendesha Mashtaka wa Serikali mkoani hapa, Amani Mohamed.

Awali, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Simiyu, Eliya Msuya, amewambia waandishi wa habari kwamba taasisi hiyo imeweza kuokoa shilingi milioni 13.7 ambazo tayari zimegawiwa kwa wakulima wa kijiji cha Nangale.


Msuya ameongeza kuwa Mabula alipokea shilingi milioni 221 kutoka NGS Investiment Co. Ltd ya Majahida, Bariadi ili akalipe wakulima waliouza pamba kwenye AMCOS ya Mwanga kituo cha Nangale ambapo alilipa baadhi ya wakulima lakini shilingi milioni 22.5 alitoroka nazo kwenda mkoani Singida.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 24, mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo na mshitakiwa huyo amerudishwa rumande kutokana na mashitaka ya uhujumu uchumi kutokuwa na dhamana.

(Imeandikwa na Anita Balingilaki, Simiyu)


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages