Maofisa wa forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kituo cha mpakani Sirari kilichopo Tarime mkoani Mara, wamekamata shehena ya vitenge vilivyokuwa vikiingizwa nchini kwa njia za magendo/panya kutokea nchini Kenya.
Vitenge hivyo vilivyokamatwa jana Juni 22, 2020 ni mafurushi (bales) 222 yenye mita 143,524, vyenye tamani ya shilingi milioni 136.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, mhandisi Mtemi Msafiri |
Kufuatia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhandisi Mtemi Msafiri, amewakumbusha wafanyabiashara kujenga utamaduni wa kusafirisha bidhaa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Serikali ili kuepuka hasara zisizo za lazima.#maraonlinenewsupdate
No comments:
Post a Comment