VIONGOZI wa wilaya ya
Rorya na mkoa wa Mara, leo Juni 26, 2020 wameshiriki uzinduzi wa Hospitali ya
Halmashauri ya Wilaya hiyo ambayo sasa iko tayari kutoa huduma za matibabu kwa
wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime,
Mhandisi Mtemi Msafiri (katikati mwenye suti nyeupe) akikata utepe kuzindua
Hospitali ya Wilaya ya Rorya leo Juni 26, 2020 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Mara, Adam Malima.
Viongozi mbalimbali wa serikali na halmashauri wakiwemo madiwani wanaomaliza muda wao wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa Hospitali ya Wilaya ya Rorya |
Ujenzi wa hospitali hiyo
umegharimu shilingi bilioni 1.8 zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Tano chini
ya Rais Dkt John Magufuli, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Rorya, Charles Kitamuru Chacha.
Pichani ni viongozi mbalimbali serikali baada ya uzinduzi wa
Hospitali ya Wilaya ya Rorya
No comments:
Post a Comment