NEWS

Wednesday 1 July 2020

TCB yatoa msimamo ununuzi wa kahawa Tarime

Wakulima wakiandaa kahawa kabla ya kuiuza
BODI ya Kahawa Tanzania (TCB) imefungua msimu wa ununuzi wa kahawa katika mkoa wa Mara huku ikitupilia mbali ombi la Wakulima wa Mara Cooperative Union  (WAMACU) Litd la kepewa upendeleo wa kuwa mnunuzi pekee wa zao hilo kwa maelezo kuwa hali hiyo inaweza kuwanyima wakulima raha.



“Tumefungua msimu na yeyote anayetoa bei nzuri kwa wakulima ni ruksa. Sisi tunachotaka ni mkulima apate raha,” Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCB, Profesa Jamal Adam, ameimbia Mara Online News kwa njia ya simu jana Julai 1, 2020.

Profesa Adam amesema hadi sasa kampuni mbili zimeshapewa leseni ya kuanza kununua kahawa katika wilaya ya Tarime mkoani Mara, akizitaja kuwa ni Kijani Hai na CMS.

“Sisi tunachotaka ni mkulima apate raha iwe ni kutoka kwa Kijani Hai, au CMS, au WAMACU,” amesisitiza Kaimu Mkurugenzi huyo wa TCB.

“WAMACU akibaki mwenyewe mkulima hawezi kuwa na furaha katika mahali ambapo hakuna ushindani.,” amesema  Profesa Adam

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages