ASKARI Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) katika Mkoa wa Kipolisi TarimeRorya wakiwa katika mazoezi ya utayari wa kuhakikisha kuwa uslama na amani vinaendelea kutamalaki kipindi cha kampeni za Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwakaa huu.
Wamefanya mazoezi hayo leo Jumanne Agosti 25, 2020 katika eneo la Gamasara, nje kidogo ya mji wa Tarime mbele ya Kamishna wa Fedha na Lojistiksi wa Jeshi la Polisi, DCP Dhahiri Athuman Kidavashari.
DCP Kidavashari alifuatana na mwenyeji wake, ACP William Mkonda ambaye ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) wa Kipolisi TarimeRorya.
(Habari na picha na Mara Online News)
No comments:
Post a Comment