NEWS

Tuesday 25 August 2020

NEC yawabariki Waitara, Heche, Mwera ubunge Tarime Vijijini

Apoo Castro Tindwa
  

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewaidhinisha wanasiasa watatu kutoka vyama tofauti kugombea ubunge katika jimbo la Tarime Vijijini mkoani Mara.

 

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tarime Vijijini, Apoo Castro Tindwa, amewataja waliopitishwa baada ya kukidhi vigezo kuwa vya NEC kuwa ni Mwita Waitara (CCM), John Heche (Chadema) na Charles Mwera (ACT - Wazalendo).

 

“Nimewataka kufanya kampeni kwa amani na wasikiuke maadili ambayo wamesaini katika fomu namba 10,” Apoo ameiambia Mara Online News jioni leo Jumanne Agosti 25, 2020.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages