Wananchi wa kata ya Gorong'a wakimshangilia mgombea ubunge jimbo la Tarime vijijini kwa tiketi ya CCM Mwita Waitara leo jioni |
Mamia ya wananchi wa kata ya Gorong'a leo Jumanne Oktoba 6,2020 wamejitokeza kumsikiliza mgombea ubunge wa jimbo la Tarime vijijini kwa tiketi ya CCM Mwita Waitara ambapo Waitara pamoja na mambo mengine ameahidi kujenga vyoo katika minada mbalimbali akipata ridhaa ya wananchi kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Waitara akikagua moja ya kadi ya wanachama wa CHADEMA waliojiunga na CCM katika mkutano huo leo |
Mapema leo asubuhi Waitara aliwasili katika kitongoji cha Nyamichele, kijiji cha Nyakunguru na kusikiliza malalamiko ya wananchi wanaodai fidia ya ardhi kutoka mgodi wa North Mara na kuahidi kusadia wananchi wa eneo hilo kupata malipo yao.
Waitara akiwa Nyamichele leo mapema |
Waitara anachuana na
John Heche wa CHADEMA pamoja na Charles Mwera wa ACT-Wazalendo
No comments:
Post a Comment