NEWS

Wednesday 21 October 2020

Msimamizi Uchaguzi Tarime Mjini awaapisha mawakala

Mawakala wa vyama vya siasa wakifuatilia maelekezo ya kujaza fomu za kazi hiyo kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tarime Mjini, Elias Ntiruhungwa (hayupo pichani) leo.

 

MSIMAMIZI wa Uchaguzi Jimbo la Tarime Mjini, Elias Ntiruhungwa leo Oktoba 21, 2020 amewaapisha mawakala wa vyama vya siasa vyenye wagombea jimboni humo kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba 28, 2020.

 

Katika tukio hilo, Ntiruhungwa amewataka mawakala hao kuheshimu maadili ya kiapo hicho ikiwa ni pamoja na kutothubutu kutoa siri za uchaguzi nje ya vyumba vya kupigia kura akisema kufanya hivyo ni kosa la jinai linaloweza kusababisha mtu kushitakiwa mahakamani.

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tarime Mjini, Elias Ntiruhungwa akitoa maelekezo ya kujaza fomu kwa mawakala wa vyama vya siasa vyenye wagombea jimboni humo leo.

 
 

Msimamizi huyo na mawakala waliozungumza na Mara Online News baada ya kiapo hicho wameeleza kuridhishwa na shughuli hiyo kwa jinsi ilivyofanyika kwa utulivu.

Sehemu ya mawakala wa vyama vya siasa wakila kiapo cha kazi hiyo mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tarime Mjini, Elias Ntiruhungwa (hayupo pichani) leo. (Picha zote na Peter Hezron)

 

Kwa mujibu wa Ntiruhungwa, maandalizi ya uchaguzi huo yamekamilika katika jimbo la Tarime Mjini ambako vimetengwa vituo 181 kwa ajili ya kupigia kura.

 

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages