NEWS

Saturday 19 December 2020

Patricia Kabaka ataka Mara Online News kuibua fursa za kiuchumi zikiwemo za ujasiriamali Mara

Patricia Kabaka

 

ALIYEKUWA Mgombea Ubunge Viti Maalum Mkoa wa Mara kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patricia Kabaka, ameupongeza uongozi wa Taasisi ya Mara Online kwa kuanzisha na kuzindua chombo cha habari cha kidijitali, yaani Blogu ya Mara Online News kwa ajili ya kutangaza fursa mbalimbali za maendeleo ya kijamii na kiuchumi zikiwemo za ujasiriamali mkoani Mara.

 

Kada huyo kijana wa CCM ametoa pongezi hizo siku chache baada ya Blogu ya Mara Online News kuzinduliwa mjini Tarime na Mkuu wa Mlkoa wa Mara, Adam Malima, huku Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Chomete akiwa mgeni rasmi.

 

Baadhi ya washiriki katika uzinduzi wa Blogu ya Mara Online News.

“Napenda kuchukua fursa hii kuushukuru uongozi wa Blog ya Mara Online News kwa kuzindua chombo hiki cha habari cha kidijitali kwani kwa dunia ya sasa ya sayansi na teknolojia jamii inahitaji vyombo kama hivi ili kuweza kwenda sambamba na mabadiliko ya sasa.

 

“Ninatoa wito kwa vijana na kina mama katika mkoa wa Mara kutumia chombo hiki kwa ajili ya kujitangazia shughuli mbalimbali za ujasiriamali ili kuweza kupanua masoko ya bidhaa zao.

 

“Ni wazi mkoa wa Mara umebarikiwa kuwa na fursa nyingi, hivyo kupitia chombo hiki cha habari makundi mbalimbali ya vijana na kina mama yataweza kupata fursa nzuri ya kusonga mbele kiuchumi.

 

"Lakini pia mkoa wa Mara tumepata chombo (Mara Online News) ambacho sasa kitatutangazia vivutio mbalimbali vilivyoko mkoani kwetu ili kuweza kuvutia watalii mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kuja mkoani kwetu na hatimaye kukuza uchumi katika mkoa wetu na hata Tanzania kwa ujumla,” amesema Kabaka.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (mwenye kofia katikati), Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Simon Odunga (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhandisi Mtemi Msafiri (wa pili kusshoto), Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Daniel Komote (wa tatu kushoto), Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Chomete (kulia), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mara Online, Jacob Mugini (wa pili kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Thobias Ghati wakipiga na kushangilia baada ya mtoto Angel Jacob Mugini kukata utepe wa uzinduzi wa Blogu ya Mara Online News mjini Tarime, Desemba 15, 2020.

 

Blogu ya Mara Online News imezinduliwa Desemba 15, 2020 ikiwa na kaulimbiu inayosema “Habari za Kidijitali kwa Maendeleo na Uhifadhi.”

Baadhi ya wafanyakazi wa Mara Online News katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa blogu hiyo. Kutoka kulia ni Christopher Gamaina, Joffrey John, Winnie Magaria, Veronica Charles, Grace Simon na Lilian Tesha.

 

#MaraOnlineNewsUpdates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages